"Lishe Bora ni Dawa. Asiye Amini Hajawahi kutendewa maajabu na Lishe bora"
Nilipokuwa mdogo sana kama miaka 10 nilikuwa naishi na bibi yangu huko usukumani Geita. Bibi yangu alikuwa ni mwalimu hivyo sisi wajukuu zake ilikuwa ni sehemu ya mfano kuhakikisha wajukuu zake tunakuwa na ufaulu mzuri sana darasani.
Unajua nini?.......Hahaha....Bibi yangu alikuwa ananitania mimi ni "Mdadisi sana" kwa sasa unaweza kunitania kwamba mimi ni "Mtafiti sana". Nilikuwa nikikaa karibu na Bibi yangu yaani "Maswali yangu ya kutaka kujua kitu yalikuwa mengi sana mpaka yana mkera sana Bibi yangu. Mwisho wa siku namwambia ...Bibi usinichukie nataka Kufahamu zaidi.
......... Siku moja nilimuuliza bibi yangu......Hivi bibi "Ugonjwa wa kisukari unatokana na nini"? Akaniuliza kwa nini umeniuliza hivyo?
Nilimjibu......Nilihisi unavyo nichapa nikiramba sukari labda nitapata ugonjwa wa kisukari nimemsikia mwalimu anasema ugonjwa wa kisukari.....Nikadhani labda ndiyo maana unanipiga...! Unanikinga na huu ugonjwa.
......Bibi yangu alicheka sana.....
.....Hahahaha.....Unajua alinijibu nini? .......Bibi alisema "Kula sukari nyingi hakuleti kisukari ila kula vitu vya mafuta na chumvi kunaleta kisukari"........................Ina maana kumbe ...Bibi alinichapa ninapokula ile sukari kwa sababu naharibu bajeti siyo kwamba najihatarisha kupata kisukari. Yeye maadui anao wajua ni Mafuta na Chumvi tu.
Bado nikaendelea na utafiti wangu. Nikawa kila nikisoma maadui wa ugonjwa wa kisukari wanaotajwa ni Mafuta yanayo ganda na Chumvi tu. Hawa ndiyo maadui wakubwa waliokuwa wanatuhumiwa toka napata utambuzi wa kuhoji mambo. Bibi yangu pia ilinielimisha hivyo.
Chakushangaza.....Sikuwahi kuona matokeo mazuri kwa wagonjwa wangu pindi nilipokuwa natumia elimu aliyonifundisha bibi yangu na elimu niliyo fundishwa katika masomo yangu yote ya elimu ya juu ya udaktari.
Nikawa najiuliza....
Hivi inawezekana kweli kuna ukweli umefichwa juu ya ugonjwa huu wa kisukari? Kwa nini elimu niliyo nayo imegoma kutoa msaada wa haraka kunusuru nguvu kazi ya taifa inayo potea kila siku kwa sababu ya ulemavu unaosababishwa na ugonjwa wa kisukari?
Huu ni ugonjwa unaotokana na uchakavu wa seli za mwili (Insulin resistance) kushindwa kutumia sukari kama ilivyo kawaida. Lakini pia ugonjwa huu unaweza kusababishwa na Kupungua kwa wingi wa maji yaitwayo Insulin ambayo ni homoni husaidia kuelekeza seli za mwili zitumie sukari.
Hivyo Ugonjwa huu unaweza ukaupata hata kama kongosho lako linazalisha homoni ya insulin yakutosha lakini kama tu kwenye kiwili wili yaani seli za mwili kuna uchakavu lazima upigwe na kisukari. Asilimia 95 ya watu wengi wenye kisukari aina hii ya ugonjwa husababishwa na Insulin kutokufanya kazi yake ya kuelekeza seli zako zitumie sukari. Na asilimia ndogo sana ya watu wote duniani wenye kisukari ugonjwa huo huwa umetokea kwa sababu ya upungufu wa homoni ya insulin.
Naendelea Kukazia maarifa Usiwe na haraka Leo somo hili ukielewa kisukari Kitakuwa kimepata mwarobaini wake nakwambia;
Asilimia 95 ya watu wote wenye kisukari duniani hawana upungufu wa insulin mwilini. Homoni ipo nyingi tena kupita kiasi ila haiwezi kufanya kazi yake ya kuelekeza seli zitumie sukari kwa sababu kuna uchakavu katika seli uliojengeka miaka mingi yaani Insulin Resistance.
Namaanisha;
Asilimia 95 ya wenye kisukari hawana upungufu wa Insulin na Kongosho huwa bado linatema insulin tena kwa wingi kuliko hata mtu ambaye hana kisukari.
Namaanisha;
Asilimia 5% tu ya wenye kisukari ndiyo hupatwa na kisukari kwa sababu ya Upungufu wa Insulin mwilini kwa sababu ya hitilafu iliyotokea katika seli zinazo zalisha hiyo homoni inayo elekeza seli za mwili zitumie sukari.
Kumbe... Ile dawa unayo ambiwa inatibu Kongosho na kuongeza uzalishwaji wa Homoni ya insulin inakusaidiaje? wakati wewe hauna upungufu wa insulin mwilini?
Kiufupi:
Ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa wa Uchakavu wa mwili mzima. Na endapo tunataka kutibu ugonjwa huu yatupasa tupate Tiba ambayo inaufanyia mwili matengenezo wote. Kwa sababu Ugonjwa wa Kisukari sio ugonjwa wa hitilafu ya kiungo kimoja bali ni uchakavu wa mwili mzima.
Je kati ya sukari na Chumvi nani adui mkubwa kwa Mgonjwa mwenye kisukari?
Jibu langu litakuwa na Maelezo kidogo.
Kisayansi katika kila lita ya damu kuna chumvi gramu 5. Binadamu hukadiliwa kuwa na wastani wa lita 5 za damu. Ina maana kiasi cha madini ya chumvi kwenye damu huwa ni gramu 15 kwenye lita 5 za damu.
Na
Kisayansi katika lita 5 za damu kiasi cha sukari hukadiliwa kuwa ni gramu 5 tu. Ambayo ni sawa na sukari kusoma 5.6mmol/L au 100mg/dl. Ina maana Chumvi katika mazingira ya kiafya huwa ni nyingi kwenye damu kuliko sukari.
.............Chumvi Huwezi kuila kupindukia,Sukari unaweza kuila kupindukia
.............Chumvi peke yake bila kitu chochote kingine hainenepeshi ila sukari ukila peke yake bila chochote unanenepa
..........Chumvi haileti Uraibu yaani addictions Lakini Sukari inaleta utegemezi (Uraibu) na usitambue kama ina kudhuru
.......Sukari inahamasisha uhifadhi wa mafuta mwilini na kuufanya mwili ung'ang'anie madini chumvi na maji mwilini.
Ina maana Chumvi huwa inatuhumiwa kusababisha shinikizo la juu la damu kwa sababu ya ubaya unaofanywa na sukari. Chumvi ni Kiungo ambacho hakina hatia kabisa.
"Hakuna binadamu ambaye anaweza kula chumvi zaidi ya kipimo maana chumvi inakera sana kwenye ulimi na ukizidisha unapata dalili palepale. Ila kuna watu wengi tu wanaweza kula sukari nyingi matokeo yake ni burudani na madhara yake huonekana baada ya miaka"
Watu wengi wanaumwa kwa sababu ya matumizi mabaya ya sukari. Vyakula vya sukari ni moja ya Vyakula vinavyoweza kumchakaza mtu akazeeka mapema na akapatwa na ugonjwa wa kisukari. Hivyo Chumvi haileti wala haipandishi sukari ya damu bali sukari inaleta na inapandisha sukari ya damu.
Wanasayansi hadi sasa tunaamini kwamba "Sukari ndiyo sumu pekee inayo mdhuru binadamu polepole bila kujua na madhara yake tiba bado ni kitendawili"
Kutokujua mwili wako haupatani na aina gani ya vyakula ungelijua ungeviepuka.
Wengi huwa na fikra hasi kwamba wamepata kisukari kwa sababu babu,bibi,mama,baba au ndugu wa karibu wana kisukari wakimaanisha wamerithi. Magonjwa kama kisukari huwa haturithi. Ukisoma kwa kina elimu ya Epigenetics (Elimu ya uhusiano wa Genes za mwili na mazingira) utagundua kwamba huwezi kupatwa na magonjwa endapo Ukiujulia mwili wako. Kinachofanya magonjwa yatembee kwenye ukoo ni kurithishana mfumo uleule wa maisha na lishe. Na kwa sababu wote mko na muundo mmoja wa mwili basi ni rahisi kuibua magonjwa yanayo watesa ukoo mzima.
Kuruhusu uzito mkubwa au kuwa na mafuta ya ziada kuliko kuzidi kiwango salama cha mwisho cha mafuta mwilini. Kitalamu kiwango cha mwisho cha mafuta mwilini huitwa Fat threshold level kiwango hiki kikipita magonjwa huanza kuibuka. Mafuta yoyote ya ziada mwilini hufubaisha sana mwili na Kukuhatarisha kupatwa na magonjwa ya uchakavu wa seli za mwili uitwao Insulin resistance. Uzito mkubwa husababishwa na matumizi ya pombe kupindukia,Unywaji wa vimiminika vyenye sukari sana,kukosa muda wa mazoezi ya mwili na matumizi ya baadhi ya dawa za kuzima kinga ya mwili steroids na zinginezo zenye tabia ya kunenepesha.
Mwili kuwa katika Msongo wa sumu zitokanazo na mfumo wa maisha Moshi wa sigara au Sumu zitokanazo na vyakula hasa vya kukaanga na mafuta dhaifu.
Kitalamu mafuta yanapokuwa yanatokota huzalisha sumu nyingi ziitwazo free radicals ambazo zinapokuwa nyingi sana huathiri viungo vya mwili na kuchakaza seli za mwili. Ni rahisi sana kupatwa na kisukari endapo mwili wako ukiuruhusu kuwa katika mazingira ya mzio sugu kwa muda mrefu. Uvutaji wa sigara huingiza mabilioni ya sumu hizi Free radicals ambazo huenda kuchakaza seli za mwili na kukuhatarisha kupatwa na kisukari.
Mwili kuwa katika Msongo wa sumu zitokanazo na mfumo wa maisha Moshi wa sigara au Sumu zitokanazo na vyakula hasa vya kukaanga na mafuta dhaifu.
Kitalamu mafuta yanapokuwa yanatokota huzalisha sumu nyingi ziitwazo free radicals ambazo zinapokuwa nyingi sana huathiri viungo vya mwili na kuchakaza seli za mwili. Ni rahisi sana kupatwa na kisukari endapo mwili wako ukiuruhusu kuwa katika mazingira ya mzio sugu kwa muda mrefu. Uvutaji wa sigara huingiza mabilioni ya sumu hizi Free radicals ambazo huenda kuchakaza seli za mwili na kukuhatarisha kupatwa na kisukari.
Matumizi ya dawa zenye tabia ya kufubaisha seli za mwili na kuathiri homoni zenye uwezo wa kuratibu matumizi ya sukari mwilini.
Kuna watu hutumia dawa za allergy predinisolone,Hydrocortisone,Dexamethasone na nyinginezo kwa muda mrefu.Dawa hizi huwa zina tabia ya kupunguzia uwezo seli za mwili wako kupokea sukari. Hali hii inaweza kusababisha Kupatwa na Kisukari hata katika umri mdogo. Pia matumizi ya vidonge vya homoni kama estrogen na Progesterone kwa muda mrefu huweza kuwahatarisha baadhi ya wanawake kupatwa na ugonjwa wa kisukari.
Kinacho nishangaza ni kwamba.....
Ni takribani asilimia 95% ya wagonjwa ambao huwa nawapokea hospitali huwa wameupotezea ugonjwa wa kisukari.
Yaaani..................
Kuupotezea namaanisha kwamba Mgonjwa ana achana nao (Ugonjwa) kuufuatilia anaamua kuishi maisha yake kama hana kisukari. Ni hatari na Kosa kubwa sana Kuchukua maamuzi mabaya kama haya.
.....Pima sukari kila siku, Mwoneshe Daktari majibu yako....Ili yeye ndiye atakaye kushauri nini kifanyike ili uweze kudhibiti ugonjwa wa kisukari.
Wamepata madhara makubwa katika mishipa ya damu.
Wengi hawafahamu kwamba kisukari ni ugonjwa wa mishipa ya damu. Huathiri karibia kila mshipa wa damu mwilini. Magonjwa haya huwatesa wengi Shinikizo la juu la damu,Kiharusi,Kutoweza kabisa kushiriki tendo la ndoa,Uono hafifu wa macho na vidonda visivyopona
Mwili kuwaka moto na Misuli kuuma sana
Hili tatizo wengi hushindwa kujua kama ni kisukari au ni ugonjwa mwilini. Ugonjwa huu usipodhibitiwa huathiri sana mwenendo wa utendaji wa mwili. Maumivu ya Joint,mifupa na misuli kuuma yote yanatibiwa kwa kudhibiti ugonjwa wa kisukari
Ogani za mwili zinakuwa zimechakaa na zingine zimekufa kabisa kiutendaji
Figo unakuta haichuji vizuri uchafu creatinine,urea na uric acidi ziko juu sana. Kupatwa na shambulio la moyo na ubongo. Yote hayo ni maafa mabaya sana kwenye mwili wako endapo ukiyaruhusu yatokee kwa kupuuza ugonjwa wa kisukari.
Wana ndoa hugombanishwa na Ugonjwa wa kisukari
Ugonjwa huu huathiri wingi wa mbegu na ubora wa mbegu kwa mwanaume. Lakini pia huathiri mayai kukomaa na Ubora wa mayai. Siyo hivyo tu huathiri uwezo wa mwanaume na mwanamke kuwa na matamanio ya kushiriki tendo la ndoa. Hali hii husumbua sana wanandoa kama mmoja wapo ana ugonjwa wa kisukari.
Kuwa na gesi kiungulia na Mwili kuwaka moto sana na wengine huwa wanakuja na dalili za magonjwa ya mfumo wa hewa
Gesi kiungulia ni dalili mojawapo kuwa sukari haijadhibitika jaribu kujitahidi kuufuatilia ugonjwa kwa ukaribu bila kupuuza matibabu unayopewa na watalamu.
Kisukari ni ugonjwa wa urithi hivyo ishi maisha yako acha kupangiwa
Kisukari ni ugonjwa unaoweza kutibiwa kwa vidonge na mizizi bila kuzingatia lishe bora
Kisukari ni ugonjwa usiodhibitika ukisha gundulika utaendelea kuteseka maisha yako yote
Kisukari ni ugonjwa wa Kitajiri na uzeeni.Asilimia kubwa wenye kisukari sasa
Kupima mara kwa mara kunatia hasira na kunatia msongo wa mawazo
Vyakula vya wanga ndiyo muhimu kukupa nguvu. Kuliko nyama samaki kuku nk
Unaweza ukaendelea kula vyakula vya wanga ila kwa uchache na bado ugonjwa wa kisukari ukawa umedhibitika
Kuna siku moja baba mmoja aliingia kwenye chumba changu cha Daktari akaanza na swali gumu sana ambalo alitaka jibu lake limpe matumaini mapya.
Aliniuliza swali hivi......
Mimi Nimeugua miaka zaidi ya 20 ugonjwa wa kisukari. Nimetembea nchi zote duniani kwa kutumia pesa zangu na cheo changu ambacho Mungu alinijalia. Matembezi yangu yote katika hospitali zote zenye hadhi ya huduma za kibingwa sikuweza kupata kupata Tiba ya kuponyesha Kisukari. Je wewe una jipya gani? Ambalo ni Tofauti na wote niliowatembelea?
Jibu langu lilikuwa kwamba;....
Hukuweza kufikia malengo kwa sababu wewe ulikuwa unatafuta dawa itakayokusaidia uppone kisukari na uendelee kufurahia vyakula kama awali.
Akasema...Ndicho nilicho Hitaji na hapa ndicho kilicho nileta.... Nikatabasamu....Hahahaha (akacheka).
Nikamwambia inawezekana;
Hata nitakapo kusaidia Ukarudi kama awali endapo ukirudia mtindo na lishe ambayo ina athiri seli za mwili kiutendaji ni Lazima Utapatwa tena na Kisukari.
Hata mimi.....Dr Boaz niko hatarini kupata Kisukari....Ila kwa sababu ninafahamu niko hatarini najitahidi sana kuepuka lishe na mtindo wa maisha ambao unaweza niletea kisukari.
Neno CURE ni kitendo cha kutibu ugonjwa kwa kuangamiza kabisa visababishi vya ugonjwa bila kuacha hata chembe. Neno hili linatumika katika magonjwa ya kuambukiza au Kuambukizwa kama Kifua kikuu,Malaria,Typhoid,Amiba nk. Tunasema nime "CURE AMOEBIASIS", Nime "CURE Malaria", Malaria ni CURABLE disease. Huwezi Kusema "Nime CURE obesity, Nime CURE Diabetes Huwezi".... Kosa la wengi hutaka kutumia neno Cure hata anapo zungumzia kuhusu magonjwa sugu ya lishe.
Huwezi kusema "Diabetes is Incurable". Huwezi Kusema "Obesity is Incurable"
Huu ni msamiati wa kitabibu ambao humaanisha kwamba tatizo Limetokea na ukiamua kuzingatia kanuni na masharti ya mwili unavyotaka hayo magonjwa yote yanapotea kabisa unarudi kama Mwanzo. Ndiyo maana nina imani kwamba "We can put Diabetes into remission", We can reverse Obesity"... Nikimaanisha ugonjwa wowote wa Lishe Hutolewa mwilini kwa Kubadilisha Mfumo wa maisha na Lishe. Ukifanya hivyo Ugonjwa unapotea wenyewe. Unakuwa kama mtu ambaye hajawahi kuwa mgonjwa.
Hakuna magonjwa yatokanayo na uchakavu wa mwili yanaweza kuitwa Magonjwa sugu yasiyopona
Magonjwa ya lishe yanaweza kudhibitika hadi ukafika hatua kukawa hakuna tena ushahidi wowote wa vipimo vya Kitalamu .
Ni kitendo cha kuondoa dalili za ugonjwa wa lishe unao kusumbua kwa asilimia flani LAKINI bado ukawa unaonekana kwenye Vipimo vikubwa ugonjwa bado unakutafuna ndani kwa ndani. Mfano unaweza kusema Ugonjwa wa Kisukari sasa umeondoka kwa asilimia 50%, Kwa asilimia 75% Lakini siyo Asilimia 100. Watu wengi ambao Hujinadi wametumia dawa za asili na Kupona kisukari huwa wanaangukiwa kwenye kundi hili. Kwa sababu ninapo wapima Kipimo kikubwa cha sukari huwa nawagundua bado ugonjwa upo na unamuumiza kimya kimya ndani. Wengi hukosea hufanikiwa kudhibiti kisukari lakini huendelea kula vyakula vilevile vilivyo wauguza kisukari. Kosa kubwa sana..
Ni kitendo cha kuondoa dalili za ugonjwa wa lishe unaokusumbua kwa asilimia 100. Hata Unapo enda hospitali vipimo vidogo vya kisukari kama Random na Fasting Blood glucose vinakuonesha wewe huna Kisukari. Na Ukipimwa pia vipimo vikubwa kama Glycosylated Hemoglobin HBA1C nacho pia kitakuonesha udhibiti wako wa sukari Upo kati ya 4% hadi 5.6%. Kwa lugha nyepesi sasa tunasema Ugonjwa Umepotea kwa sababu hakuna ushahidi wa dalili,Hakuna ushahidi wa Vipimo vidogo na Hakuna ushahidi wa vipimo Vikubwa. Unawezaje kumuita mtu ana Kitambi wakati hana kitambi? Unamuitaje mtu ana kisukari wakati vipimo vyote havioneshi?
Ingelikuwa umeambiwa, una elimu au Ingekuwa kuna mashine ya kupima mwili mzima ukapewa ripoti kuwa seli zako za mwili hazipendi mazingira Flani katika mwili wako. Na Ukatahadharishwa. Nakuhakikishia Usingepata Kisukari.
Watu wengi hupatwa na Ugonjwa wa Kisukari kwa Kukosa Elimu ya Lishe toka anapozaliwa mpaka anapata Kisukari.
Wengi huwa wanakula,Wanakunywa na Kuishi maisha ya starehe katika kiwango cha furaha wanavyo jisikia kuishi. Ugonjwa wa Kisukari hutokea kama Umeshitukiza au umekuja kuharibu starehe zake za kila siku.
Lakini Ujumbe wangu kwako ni kwamba;
"Elimu hii nitakayokupa Leo siyo kwa ajili ya kudhibiti Kisukari tu lakini ndivyo unavyotakiwa kuishi kulingana na muundo wa mwili wako kibaolojia.
Malezi ya tangu utotoni huathiri wengi sana wanashindwa kuja kubadilisha mfumo wa lishe ambao wamezoea kula hivyo toka alipozaliwa.
Uraibu wa vyakula huwatawala wengi wanakosa mamlaka juu ya mwili wake. Unakuta mtu vyakula vimemuathiri kwelikweli na Ugonjwa wa kisukari umempiga kwelikweli. Ila kwa sababu vyakula Vimemletea uraibu (Addictions) kama mtumiaji wa madawa ya kulevya basi hawezi kuacha vyakula hivyo.
Watu wengi hawajui kula kulingana na baolojia ya mwili wake.
Hata kama anaonekana kuongezeka sana huwa hawajihoji hitilafu gani imetokea mwilini na imesababishwa na nini mpaka uzito umefikia hatua mbaya.
Hii ni moja ya sababu inayofanya ugonjwa mmoja unawatafuna ukoo mzima. Kwa sababu nyie wote mnafanana muundo wa mwili kibaolojia na kinacho waathiri ukoo mzima ni kitu kilekile.
Msipo kitambua na kukiepuka utashangaa kila mtu kwenye ukoo wenu akazikwa kwa sababu ya Kisukari
Hata wewe kutokujua kula kulingana na mwili wako unavyotakiwa kulishwa ni moja ya sababu kwa nini umepatwa na ugonjwa wa kisukari
Kula kulingana na aina ya kazi yako na Kiwango cha mazoezi.
Huwezi ukawa ni mtu wa ofisini tu muda wote halafu wewe unakula milo 3-6 kwa siku na milo yote haizingatii Misingi ya lishe bora.
Na bado ukiwa kazini una kimiminika chenye sukari nyingi,ladha na kemikali zinazo athiri usafi wa damu na mwenendo wa seli zako.
Ukitoka hapo unapita Bar kama wewe ni mnywaji maana huwa unajinadi wewe sio mlevi. Ukifika huko tena unajipunguzia umri wa kuishi bila magonjwa ya lishe kwa pombe chupa kadhaa.
Hii ni sababu kubwa sana vijana wadogo chini ya miaka 35 wanapigwa na Kisukari hata kama ukoo wenu Hakuna mwenye Kisukari.
Kukosa Tabia ya Nidhamu ya lishe bora katika maisha yako ya Ujana wako.
Kukosa nidhamu ya lishe bora ni pale ambapo mtu anakuwa na visingizio vingi vya kutokufuata lishe bora.
Visingizio ni pamoja na aina ya kazi anayofanya inambana kula kiafya, Mazingira ya kazi yake hakuna chakula bora hivyo hawezi kula kiafya.
Nikwambie kitu Siku ukianza kuugua kila siku hiyo kazi wataichukua wale wenye nidhamu ya lishe bora.
Endelea kuruhusu fikra hasi hizo zimeumiza wengi na wako kwenye majuto ya kupoteza kazi na wanaishi na magonjwa sugu ya lishe ambayo hawawezi hata kujitibia sababu wamepoteza kazi.
Hata umiliki mali nyingi duniani bila afya njema huhatarisha kifo kwa watu wengi kwa sababu ya Msongo mkubwa wa kutokuzitumia wakati walizitafuta.
Ilikuwa mwaka 2015 baada ya kuhitimu masomo yangu ya Udaktari Doctor of Medicine(MD) chuo kikuu CUHAS-Bugando. Nikiwa niko kwenye mafunzo ya vitendo Internship Mwananyamala Hospitali (Hospitali ya Rufaa Kinondoni).
Nilijifunza mambo mengi ambayo Yaliniumiza sana sitaki wewe Upitie kabisa;
Nilipokuwa Wodi ya Mama mjamzito na waliojifungua. Nilijifunza Kuna kisukari hutokea wakati wa Mimba. Hasa mimba inapokuwa imefikisha Wiki kuanzia 28 yaani Miezi 7.
Aina hii ya Kisukari mama huambiwa ni kisukari cha mimba tu baada ya kujifungua hupotea.... Daktari akimuaminisha mgonjwa kilicholeta kisukari ni Mimba aliyobeba. Ni Uongo nakwambia...!
Kisukari ni Ugonjwa ambao hujitengeneza kwa miaka 5-10 ndapo unajitokeza. Siyo ugonjwa unaoweza kujitengeneza ndani ya wiki 28 ukapata. Mwanamke yeyote anayepatwa na Kisukari wakati wa mimba huwa tayari amesha jiuguza kutokana na mfumo wake wa maisha kabla ya mimba. Kitalamu anakuwa yupo kwenye hatua za awali ugonjwa ukiwa unajitengeneza tunaita Pre diabetic stage.
Unaweza kuishi na hali ya kisukari kilicho jificha bila kujitambua hata miaka 2 hadi 5. Ila pale itakapo tokea tu kuna kitu kinacho chokoza mwili wako ukatikisika ugonjwa utajionesha waziwazi.
Kitalamu wakati wa Mimba. Yale mabadiliko ya homoni yanayo tokea wakati wa kulea mimba huathiri uwezo wa mwili kutumia sukari na matokeo yake uhatari wa kupata kisukari ni mkubwa sana.
Kuna homoni iitwayo Ant Mullerian Hormone (AMH), hii ni homoni ambayo husaidia mtoto apate kwanza lishe kabla ya seli zako za mama hazipata chakula. Hali hiyo hufanya mwili wako upunguziwe uwezo wa kupokea chakula na mahitaji mengine hadi mtoto apate kwanza chakula. Kupungua kwa uwezo huo unaweza kukufanya kuanza kupata dalili za kisukari na hata kuibua kisukari kabisa kama ulibeba mimba ukiwa hatua za kisukari kilicho jificha.
Ushawahi kumuona mama akibeba mimba anakuwa mweusi zaidi? Ushawahi kuona mama akibeba mimba anapata visunzua vingi sana? Ushawahi kusikia mama amebeba mimba amepata kisukari? Yote hayo yanapotokea. Mimba isipate lawama.
Anayetakiwa kulaumiwa ni wewe mwanamke umebeba mimba wakati mazingira ya ndani sio salama kiafya. Kama mwanamke yuko salama hayo mabadiliko ya homoni zinazo mlea mtoto hayawezi kuleta dalili za kisukari pre diabetes na wala Kisukari.
Kisukari kilicho Jificha wakati wa mimba ni hatari sana humhatarisha mama kupata mtoto mkubwa kupita kiasi Big baby, Mtoto kufia tumboni (Intra uterine Fetal death),Mama kuwa anapoteza mimba kila anapobeba inamwagika ndani ya wiki chache tu,Mwanamke kupatwa na kifafa cha mimba,Mwanamke akifanyiwa upasuaji kidonda huchelewa kupona na nyuzi huachia uhatari wa kufumuka kwa tumbo na kuoza sehemu iliyo chanwa ni mkubwa sana. Kiufupi Ugonjwa huu ni hatari sana na bado wanawake wengi hawajui kama upo na kama hutokea wakati wa mimba.
Asilimia kubwa ya wanawake wengi wanao beba mimba wanapata kisukari na baada ya kujifungua ugonjwa hupotea. Lakini ukimpima vipimo vikubwa vinakuwa vina onesha huko mbeleni ugonjwa utarudi. Wengi hujisahau na ukubwani huwa ugonjwa unarudi na makali ya kivingine. Elimu ni Muhimu sana.
Hakuna kitu kilichokuwa kinaumiza kama mama anatakiwa kunyonyesha,Kufurahia mtoto wake lakini anaingia kwenye majonzi ya kulea kidonda cha upasuaji kisichokuwa na uhakika wa kupona.
Katika wodi ya watoto nilijifunza kuna Kisukari aina ya kwanza.
Kisukari kilichotokana na Kongosho kushambuliwa na mcharuko wa kinga ya mwili na kuathiri uwezo wa Kongosho kuzalisha homoni ya insulin.
Homoni ya Insulin husaidia kuelekeza seli za mwili ziweze kutumia sukari iliyopo kwenye damu ili uweze kupata nguvu.
Endapo Homoni hii ipo kidogo uwezo wa kuzielekeza seli zote za mwili zitumie sukari hupungua hivyo sukari nyingi hubaki kwenye damu na hiyo ndiyo humuathiri mtoto mpaka anagundulika na kisukari punde tu anapozaliwa au Miezi kadhaa ua miaka kadhaa toka amezaliwa.
Hakuna Kitu kinaumiza mama anapopata mtoto mwenye kisukari aina ya kwanza. Nimetibu watoto wenye kisukari waliogunduliwa wakiwa na umri wa miezi chini ya . Aisee ni kazi sana....! Kumbuka mtoto anakuwa ananyonya maziwa ya mama tu na bado sukari inasoma iko juu sana. Na Mama anatakiwa amchome sindano za insulin ili kuhakikisha sukari haipandi. Kumbuka mtoto mdogo dawa ikimzidia hawezi kujitetea kwa kuita au kupiga kelele.
Ina maana Unatakiwa muda wote uwe naye mikononi mwako. Ni stress kali sana sijapata kuona maishani na huathiri hata uwezo wa uzalishaji katika familia maana huwezi kuendelea hata na shughuli zako za biashara. Unakuwa busy Kumlea mtoto wako.
Wengi huamini kwamba kisukari cha utotoni ni mapenzi ya mwenyezi Mungu. Hapana hakuna hilo, Mungu gani anayependa wewe upate adhabu nzito hivyo maisha yako yote? Ni mapenzi yetu sisi kupuuza ushauri wa kitabibu ili kujikinga na majanga kama haya.
Mwanamke ambaye ana maradhi ya sumu nyingi zitokanazo na mfumo wake wa maisha yuko hatarini kumhatarisha mtoto aliyeyoko tumboni na mtoto akatoka ana ulemavu wa viungo mbalimbali ikiwemo kongosho.
Mwanamke mwenye Pumu ya kifua, Mwanamke mwenye allergy sugu,Mwanamke mwenye uzito mkubwa,Mwanamke anayesumbuliwa na mambo ya uzazi kwa muda bila mafanikio,mwanamke mwenye magonjwa ya kisukari kinacho julikana au kilicho jificha Yuko hatarini kuzaa mtoto mwenye hitilafu kwenye kongosho na mwenye kisukari.
Kitalamu mwanamke yeyote mwenye Allergy sugu ya mwili (Mwitikio mkali wa kinga ya mwili unaodumu kwa muda mrefu) huathiri viungo mbalimbali katika mwili na hali hiyo inaweza kumuathiri hata mtoto aliyeko tumboni.
Ninacho kiamini ni kwamba mwanamke akichukua tahadhari kabla hajabeba mimba akajiandaa vizuri (Akasafisha damu kwa kuzingatia lishe bora) kuna uwezekano wa kupunguza idadi ya watoto wanao zaliwa na kupata ugonjwa wa kisukari. Mama ndiye humuuguza Mtoto kisukari na siyo mapenzi ya Mungu.
Katika wodi ya watu wazima nilijifunza ni kazi sana kunusuru uhai wa binadamu katika hospitali zetu pale ambapo unapofikishwa na ugonjwa wa kisukari katika hatua ambayo unahitaji uangalizi wa karibu (Intensive Care Unit).
Nilishuhudia wagonjwa wakiwa ICU jinsi gani ilivyo kazi kunusuru uhai. Ugonjwa wa Kisukari huathiri ogani nyingi mwilini. Hebu fikiria sukari iko juu, Shinikizo la juu la damu,Figo zimekufa creatinine iko juu, una kidonda mguuni kina hali mbali kinakuletea homa kali kama ishara ya bakteria wamesambaa kwenye damu. Unadhani katika hali hiyo ni nafuu kunusurika?
Nilicho kichagua ni kujikita kwenye kukinga mtu yeyote asipate kisukari na Kumsaidia mtu yeyote mwenye kisukari asiruhusu uchakavu wa mwili utokee kwa sababu ya kukosa elimu au ukaidi wa kupokea elimu.
Ndiyo maana huwa sichoki kumfundisha mtu hata ambaye naona bado ana kiburi cha afya njema na uraibu wa vyakula umemtawala. Mimi huwa nina imani siku haya ninayo andika ukiyaamini tutawanusuru wengi ambao pia wataamini kupitia wewe.

Hii ni sahani itakayokupatia virutubisho vyote vya muhimu kwa ajili ya kufanya matengenezo ya mwili. Pia sahani hii itakusaidia kudhibiti wingi wa sukari. Kitu kikubwa tunacho kizingatia ni mgonjwa aweze kufurahia mpangilio wake wa lishe bora na aweze kuona urahisi wa kutekeleza programu kwa miezi angalau 6 mpaka 8
Moja ya kitu kikubwa ambacho kinasababisha madhara makubwa ya kisukari kwa mgonjwa mwenye kisukari ni mgonjwa wa kisukari asiye zingatia lishe bora.
Ushawahi kushauriwa...Zingatia dawa zako tu kula chochote? Anakuangamiza!
Ushawahi kushauriwa...Mgonjwa wa kisukari hutakiwi kuwa mpangilio wa lishe wa tofauti na familia yako na ukashauriwa ule chakula kilekile wanachokula wengine ila tu upunguze kiwango? Anakuangamiza!
Ushawahi kuambiwa ule vyakula vya wanga kwa kipimo cha ukubwa wa ngumi? Ushawahi kuambiwa Viazi,Magimbi,Ndizi ngumu,mtama,mahindi ya njano,Ngano nzima,mchele wa brown havipandishi sukari ni mbadala mzuri wa wali mweupe na ngano nyeupe? Anakuangamiza.
Nitakupa fomula nzuri namna ya kuunda sahani tiba itakayo kusaidia kudhibiti kisukari. Nakuhakikishia utashiba,utafurahia mfumo wangu wa lishe na utapona magonjwa yanayo kusumbua.
Wagonjwa wengi wenye kisukari hushangaa kwa nini hata wakati ambao hawajala kitu cha sukari kwa siku kadhaa wakiwa kwenye mfungo bado kiwango cha sukari huonekana hakipo kwenye kiwango salama? Hii ni kwa sababu binadamu huwa tuna chanzo cha sukari mwilini kiitwacho Ini.
Ini la binadamu ambaye hana ugonjwa wa kisukari huzalisha sukari pale ambapo kuna uhaba wa sukari katika damu. Labda umekaa muda mrefu hujala chakula chochote ili sukari isishuke ukapoteza maisha kuna Kiungo mwilini kinaitwa Ini husaidia kuweka sukari katika kiwango salama muda wote hadi pale utakapo kula. Ina maana Ini hutunusuru na Kifo kwa kututengenezea sukari mwilini.
Ini la binadamu lina uwezo wa kuzalisha sukari hadi gramu 200 ndani ya masaa 24 endapo hujala kitu chochote.
Ndiyo maana unaweza kusafiri zaidi ya masaa 20 bila kula na ukafika salama. Kiufupi Ini ni kiwanda cha sukari kinacho fanya kazi pale tu kunapokuwa hakuna sukari inayo ingia kutoka nje na seli zako za mwili zikawa zina uhitaji wa sukari. Ini Hupumzika kutema sukari pale unapo ingiza sukari kutoka nje.
Sasa unapokuwa mgonjwa wa kisukari hasira ya Ini kutengeneza sukari na kuimwaga kwenye damu huongezeka kwa kikubwa sana. Hali hiyo husababishwa na idadi kubwa ya seli za mwili zenye uchakavu.
Ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa wa uchakavu wa seli za mwili, Ni ugonjwa unao piga na kuharibu karibu kila aina ya kiungo kwenye mwili wa binadamu. Sasa baada ya kudhibiti vyanzo vyote viwili vya sukari hatua inayofuata ni kutengeneza mazingira mazuri ili seli mpya ambazo huzaliwa kila sekunde zisiweze kuathiriwa na sumu au wingi wa sukari nazo zikachakaa yaani zikawa Insulin resistant.
Ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa unaotokea kwa sababu ya uchakavu wa seli za mwili. Na aliye fubaza seli za mwili ni wewe wakati unaishi bila utambuzi nini kinacho endelea wakati unakula na kunywa. Ugonjwa haina maana kwamba Seli zako za mwili zitakuwa zinazaliwa au huzaliwa zikiwa hazina uwezo wa kufyonza sukari moja kwa moja. Hapana. Seli zako zitakuwa zinazaliwa zikiwa nzima kabisa Insulin sensitive lakini kama mazingira ya mwili wako hauja safisha utashangaa seli hizo mpya nazo zitafubaishwa na mazingira machafu ya mwili ambayo hujayashughulikia.
Ndiyo maana Fomula yangu ina nguvu sana na wengi wameshuhudia maajabu yake. Tunachokifanya tunazuia seli zako za mwili kufubaishwa na mazingira chakavu au mabaya yaliyo jaa sumu nyingi mwilini kwa kusafisha damu yako iwe safi.
Kisayansi kila baada ya sekunde mamilioni ya seli mpya huzalishwa mwilini. Seli hizi mpya zinakuwa ni Insulin sensitive namaanisha nzima kabisa. Na kila sekunde mamilioni ya seli humaliza muda wake wa kuishi kwenye damu hizo zinazo maliza muda ndiyo zile chakavu Insulin resistant cells. Hivyo zinapomaliza muda zinapungua zenye uchakavu na zinapoliwa mpya na tukazuia hizo mpya nazo zisifubaishwe tutakuwa tunafanya zile nzima zitawale. Kitalamu tunasema tunaongeza Insulin sensitivity na ugonjwa wa kisukari hupotea kadri mwili unavyofanya hayo matengenezo. Umeona Fomula yangu jinsi inavyofanya kazi? Nakuhakikishia Ukifuata utapata Maajabu makubwa sana.
Matengenezo hutegemea na Umri wa mtu kumbuka Kasi ya kuzalisha seli mpya kwa mtu mwenye umri chini ya miaka 45 ni kubwa sana kuliko mwenye umri mkubwa. Lakini kwa uzoefu wangu wa kutibu wagonjwa wa kisukari miaka 8 wengi hufikia hatua nzuri ya udhibiti wa sukari ndani ya miezi 8.
Yaani miezi 8 ni ile upate Complete au Full Diabetic remission lakini maendeleo mazuri ya sukari kusoma vizuri 4-5.6 huwa tunayafikia ndani ya mwezi tu yaani siku 30.
Pale Mgonjwa kila anapokuja Kliniki akapimwa sukari akiwa amekula kwa kuzingatia sahani Tiba na akiwa hajala sukari ikawa inasoma 3mmol/L hadi 5.6mmol/l.
Na akifanya kipimo cha Udhibiti wa sukari kwa miezi mitatu kipimo cha Glycosylated Hemoglobin kinasoma 4%-5.6% huku akiwa hana msaada wowote wa dawa isipokuwa lishe tu. Pia hana vipimo vyovyote vinavyo ashiria mwili wake bado uko kwenye mazingira ya sumu nyingi au dalili za madhara ya ugonjwa wa kisukari.
Mgonjwa huyu huwa tunamuweka kwenye hatua ya uangalizi wa kila baada ya miezi 6 anatakiwa kuwa anafanya uchunguzi na tunampa Fomula namna ya kuishi ili sukari isipande tena. Ugonjwa wa Kisukari ni Ugonjwa wa Lishe na mfumo wa maisha. Kuwa na imani baada ya matengenezo na ukajua jinsi ya kuishi kulingana na baolojia ya mwili wako basi ujue ugonjwa hauwezi kurudi utaishi kwa historia Ulikuwa na kisukari sasa uko kwenye Full Diabetic Remission na hakuna kipimo kinachoweza kukutafsiri wewe ni mwenye kisukari.
Sio jambo rahisi lakini kwa mwenye nia ya dhati ni rahisi sana na nimewasaidia maelfu ya watanzania kufanya maamuzi haya. Elimu hii huwa siitoi wazi hivi ila nimewiwa kuwasaidia hata ambao hawawezi kunifikia ofisini kwangu kupona ugonjwa wa kisukari. Utakayenipa ushuhuda ni yule mwenye Imani na haya mafundisho yangu.
Hakuna kitu kigumu kama kumtibu mgonjwa aliyekata tamaa. Asilimia kubwa ya wagonjwa ambao huwa nawapokea wamefirisiwa na ugonjwa wa kisukari, Wamepoteza matumaini ya maisha na wamekata tamaa. Mimi napokea wagonjwa ambao hufikia fomula yangu hii kama ni jambo la mwisho.
Unafahamu kabisa wengi hawapendi njia ndefu wengi hupenda kuambiwa tumia dawa hii uta endelea kula keki,ugali,wali ndizi yaani vyakula vyote ambavyo havipatani na mgonjwa wa kisukari. Sasa ushauri huwo wengi huona ni mzuri kuliko fomula yangu. Matokeo yake unafuu au mteremko huwaponza nakuja kuwapokea wakiwa wana hali mbaya sana.
Kisukari ni ugonjwa unaomuathiri Mgonjwa kimyakimya kama Mchimba handaki. Siku Tetemeko likitokea ndipo mtafahamu hapo uliposimama kulikuwa na handaki. Madhara ya kusukari usiya ruhusu kutokea na inapotekea usiyapokee.
Hivyo kwenye hatua hii huwa tunajitahidi kumtengeneza mtu kuweza kutupokea sisi kuendesha mfumo wake wa lishe na maisha kwa kufuata fomula zetu. Wengi wagonjwa wetu tumewajenga kifikra maana hatuwakaririshi elimu hii wana elewa elimu hii na wanajua matunda yake. Wewe pia unayedhani haiwezekani Nitabadilisha maisha yako na Utajutia kwa nini hukunifahamu au kuamini mapema.



Thamani yake 50,000 utapewa summary BURE

