Metabolic Infertility ni Ugonjwa gani?
Metabolic Infertility ni aina ya ugumba unaosababishwa na magonjwa ya lishe yanayo julikana au yasiyo julikana kumfunga mwanamke na mwanaume uwezo wa kupata mtoto.
Hivi unafahamu kwamba, unaweza ukawa hauna ugonjwa wowote unaokufanya unywe dawa kila siku na bado mwilini ukawa ni mgonjwa. Na tatizo hilo ambalo limejificha (Ugonjwa) likawa ndiyo chanzo cha wewe kutokushika mimba katika umri wako wote wa uwezo wa kuzaa. Nimekutana na wengi na nimewatibu wengi sana!
Huamini Haya? Je ushawahi kusikia haya Maishani mwako?
Amehangaika sana kubeba mimba baada ya kufanikiwa amepata kifafa cha mimba mimba ilipofikisha miezi 7 (Wiki 28) akapatwa na Eclampsia.
Amehangaika sana kubeba mimba baada ya kufanikiwa amepata Kisukari wakati mimba ina miezi 5 (Wiki20)
Amehangaika sana kubeba mimba baada ya kupata mimba mtoto hakui daktari amemua kusitisha mimba kwa kumsafisha kizazi atafute mimba mpya.
Amehangaika sana kutafuta mimba baada ya kupata mimba imefikisha miezi 5 (Wiki 20) mapigo ya moyo ya mtoto hayasikiki. Ikabainika mtoto kafia tumboni (Intra uterine Fetal death)
Amehangaika sana kutafuta mimba kila kibeba mimba hawezi kuvukisha umri wa wiki 12 miezi 3 mimba inaporomoka.
Amehangaika sana kutafuta mtoto hakufanikiwa kubeba mimba hata kidogo. Alipofikisha umri wa miaka 40 akaambiwa ana kisukari na hatimaye shinikizo la damu la juu.
Amehangaika sana kutafuta mtoto na hakufanikiwa kupata mimba kabisa baada ya kufikisha umri mkubwa zaidi ya miaka 40 amegundulika ana tatizo la tezi ya shingo Thyroid gland disorder amepangiwa upasuaji.
Amehangaika sana kutafuta mimba na hakufanikiwa kubeba mimba kabisa. Ila sasa ameambiwa ana uvimbe kwenye ubongo unaotema homoni ya prolactin na anatakiwa kusafirishwa kwenda india kwa upasuaji mkubwa.
Amehangaika kutafuta mtoto hakufanikiwa kabisa. Sasa ameambiwa kizazi chake kinatakiwa kitolewe kwa sababu kina dalili zote za kansa na kubaki nacho ni hatari kwa uhai wake.
Dada mwenye Umri wa miaka 37 alijiunga na Programu yetu,Metabolic Infertility February 2023. Alijiunga kwa sababu ya Uzito mkubwa, Aligundulika na Kisukari hivi karibuni alikuwa anatafuta mtalamu amsaidie upande kudhibiti kisukari, Hedhi Ilikuwa Imekata zaidi ya mwaka. Na alikuwa ana tafuta mtoto wa Pili kwa miaka zaidi ya 9 bila mafanikio.
Majibu ya Kuwa ana Ugonjwa wa kisukari yalimstua sana na alishangazwa sana. Alichukua maamuzi magumu kwa kujiunga na programu yangu. Alihamasika baada ya kusikiliza Mafunzo yangu ya youtube na akafikia hitimisho kwamba, Suluhisho la magonjwa yote aliyonayo sasa ni Kubadili mfumo wa Lishe yake.
Alijunga na Kifurushi chetu cha Usimamizi wa karibu One on One Online consultation maana alikuwa anaishi mkoani.Tulimuunganisha na Usimamizi wetu na akaanza rasmi Tarehe 20,Feb,2023.
Alipokuwa anaanza Programu Usugu wa Ugonjwa wa Kisukari Ulionesha Udhibiti (HBA1C) asilimia 11% ambayo ni hatua mbaya. Sukari ya siku ilikuwa inasoma zaidi ya 10. Hedhi alikuwa amefunga kabisa kwa sababu ya uzito mkubwa na kisukari kilichokuwa hakijulikani kabisa.
Alikuwa anapima Kipimo Kikubwa cha sukari aliweza kudhibiti kisukari Kutoka11% , ikaja 8.7% hadi 6.0% Bila dawa. Kwa Lishe bora ambayo nilimpatia wakati amejiunga na Metabolic infertility.
Alianza kuona hedhi ndani ya miezi miwili baada ya kuanza Mpango wangu wa Lishe bora na matibabu mengine.Alifurahi sana maana alikuwa ametumia kila aina ya dawa aweze kupata hedhi bila mafanikio.
Jana Tarehe 07.09.2023 Ametuma Ushuhuda mzito sana ameshika mimba. Kitu ambacho Anashindwa kuamini maana Mtoto wake wa kwanza ni mkubwa sana na Amekuwa akisaka mimba ya pili miaka 9 bila mafanikio.
Alibeba mimba ya kwanza wakati wa ubinti bila shida yoyote kabisa
Alipo taka mimba ya pili ndipo ikawa shughuli nzito
Amekuwa akihangaika kutafuta mtoto bila kujua kama ana kisukari
Alipotamkiwa ana kisukari ndipo alishtuka akaanza kubadili lishe yake
Baada ya kubadilisha mfumo wake wa lishe ugonjwa wa kisukari ukapotea akaanza kupata hedhi kama kawaida na akabeba mimba
Huyu alifungwa uzazi na magonjwa asiyo yajua
Kupitia programu yetu ya Metabolic infertility tumerudisha tabasamu na tumekata kiu ya yeye kupata mtoto wa pili.
Tarehe 28.05.2022 Nilipokea mgonjwa. Dada huyu alikuwa na umri wa miaka 29, Kilo 78 na urefu wa 158cm. Malalamiko yake yalikuwa ni ameolewa miaka 4 iliyopita na hajapata mimba. Hedhi yake sasa imekoma kwa miaka 3 anapata akinyweshwa Vidonge vya Progestin.
Tulipokuwa kwenye mahojiano nikamuuliza swali kwa utani “Umemaliza matatizo unayotaka nikutatulie? ... Akasema Ndiyo!
Nikamwambia mbona pua zako kama zimeziba haya mafua yameanza lini? ...Akajibu haya yapo tu nisha yazoea. Maana nishakunywa dawa za allergy mpaka basi.
Baada ya stori kidogo kimazungumzo basi nikagundua namhudumia dada yangu “From Singida”.
Nikamtania kidogo shemeji yangu (Mume wake)......hahahaha....Kiomboi,Kinampanda......Mitaa ya kwetu huko.
Basi tukaendelea na huduma ya vipimo zaidi. Sisi Nsambo Healthcare tunapo mpokea mgonjwa hapati hedhi na mimba hapati lazima tufanye Full Body checkup (Uchunguzi wa kina mwili mzima) kujua hitilafu iko wapi?
Uchunguzi wetu huhusisha;
kuangalia uhai au utendaji kazi wa tezi ya uzazi iitwayo ovari.
Baada ya kujua hivyo basi huwa tunapima kwa kina;
Kujua chanzo kwa nini ovari yake ina mwonekano huo mpaka asipate hedhi na Asibebe Mimba.
Baada ya Uchunguzi huyu dada iliyonesha;
Mayai hayapevuki vizuri alikuwa na PCOS kwani AMH ilikuwa 11.52, Alikuwa na udhibiti sio mzuri wa sukari,Pre diabetes HBA1C 6.48%, LH ilikuwa Juu. Kipimo cha Msongo wa sumu na allergy sugu kilikuwa juu sana hata mashine ilishindwa kusoma yaani hsCRP ilisoma zaidi ya 10mg/l
Baada ya uchunguzi matibabu yaliendelea na ndani ya miezi 2 alipata hedhi na kuendelea na matibabu yetu.
Hebu Fikiria amepata hedhi asili bila kupatiwa dawa yoyote ya vidonge vya progestin ambavyo huleta hedhi Feki (Artificial menstruation).
Tulimpatia Lishe ya kufuata na matibabu mengine ya kuondoa madhara ya sumu mwilini zilizokuwa zinamletea allergy sugu na kuvuruga homoni zinazo ratibu mayai kukomaa.
Kwa sababu alikuwa anaishi mikoani hatukuweza kuonana naye mpaka aliporudi kliniki tena kwa mara ya pili kwa uchunguzi kujua maendeleo yake. Amerudi Kliniki tarehe 09.09.2023.
Akiwa anapata hedhi kila mwezi,hana maumivu hata kidogo, na allergy ikiwa imepungua sana.
Baada ya vipimo ilionesha mayai yake yameanza kukomaa vizuri AMH imekuwa nzuri 4.34, LH na FSH ziko vizuri,Sukari iko vizuri HBA1C 5.59%. Tukampatia tena matibabu ya kuimarisha zaidi ubora wa mayai kwa miezi 3.
Utajifunza maana ya Metabolic Infertility
Sifa zipi zinamfanya mwanamke aitwe Mgumba?
Mzunguko wa hedhi feki na mzunguko wa hedhi asili
Hasara mwanamke unapokuwa na mzunguko feki kila mwezi
Faida mwanamke kuwa na mzunguko asili na wenye afya njema
Utajifunza maana ya mzunguko wa hedhi na sayansi yake
Jinsi ya kufuatilia mzunguko wako wa hedhi uongeze uwezekano wa kubeba mimba
Magonjwa ya mzunguko wa hedhi na namna ya kuyatibu.
Njia marufuku ambazo zimevuruga hedhi kwa wanawake wengi
Utajifunza kwa kina kazi ya ovari za mwanamke
Mambo yanayo zeesha ovari zako na kupunguza ubora wa mayai
Magonjwa ya Upevushaji wa mayai na namna ya kuyatibu
Makundi 05 ya wanawake wanao tafuta mimba ukirejea kwenye umri wa ovari
Vipimo vya kutathimini Umri wa ovari na ubora wa mayai
Yajue magonjwa zaidi ya 10 ambayo hufunga uzazi wanawake wengi.
Jinsi ya kuayabaini magonjwa hayo kwa dalili na vipimo vya kisasa vya sampuli ya damu
Jinsi ya kuyatibu magonjwa sugu yanayo watesa wengi kiafya bila ufumbuzi
Athari za magonjwa sugu. Jinsi yanavyo athiri ubora na wingi wa mayai
Utaunganishwa na Whatsapp na Telegramu group BURE. Hili ni kundi la kupata hamasa na kutiana Moyo
Utapewa Mwongozo wa Elimu ya uzazi na Lishe.Utapata nakala Ngumu Kitabu cha Sayansi ya Homoni na Ugumba
Utapewa majarida ya kukuongoza unapokuwa unatekeleza programu yetu ya lishe bora.
KATIKA METABOLIC INFERTILITY
Dr Boaz Mkumbo ni Daktari wa magonjwa ya binadamu (Doctor of medicine), Mganga mfawidhi Nsambo Healthcare Polyclinics. Mwanzilishi wa programu maarufu ya lishe bora Tanzania iitwayo Sayansi ya Mapishi. Kwa miaka 8 sasa amekuwa mkufunzi wa magonjwa ya lishe na amekuwa akitibu wagonjwa wenye magonjwa sugu ya lishe na homoni katika kituo chake kilichopo Dar es salaam Mkabala na Hospitali ya mwananyamala, Nsambo Healthcare Polyclinic.
Ni mwandishi wa kitabu cha mwongozo wa lishe bora kiitwacho Sayansi ya mapishi. Kitabu hiki kimesomwa na maelfu na maelfu ya watanzania. Yawezakuwa hata wewe ushawahi kukutana nacho ukakipuuzia lakini bado Mungu ana nia njema na wewe kukutimizia jambo lako kupitia mafunzo ya Lishe bora ya Kitabu hiki.
Mbali na Kitabu cha sayansi ya mapishi ameandika kitabu maarufu cha mwongozo wa lishe bora kwa mwanamke anayetafuta mtoto kiitwacho Sayansi ya homoni na ugumba. Kitabu hiki ndicho kimetufanya tukuandalie programu ya Metabolic infertility ili tutekeleze maarifa ya kitabu hiki kwa vitendo.
Elimu ya maarifa ya kitabu na mafunzo haya yametumiwa na maelfu ya watanzania. Wewe hautakuwa mtu wa kwanza kutekeleza mafunzo haya.
Nsambo Healthcare tumejikita kutibu magonjwa ya lishe na homoni kwa njia nyongeza ambazo zina ushahidi kisayansi.
Wanandoa waliotumia mbinu zote za matibabu kitaalamu hawakufanikiwa kupata mtoto. Na Hospitali huambiwa hawana tatizo lolote.
Wanandoa waliotumia mbinu zote za matibabu kitaalamu kila wanapopimwa huambiwa wana mvurugiko wa homoni na hawapati suluhisho la kupakata mtoto
Wana ndoa ambao mwanamke hedhi imekata na bado wako katika umri wa kuzaa chini ya miaka 45.
Wanandoa ambao mwanamke ana umri chini ya miaka 50 na bado anapata hedhi
Utapata Elimu ya kina juu ya tatizo lako la uzazi hivyo elimu itakusaidia kujua wapi unapokosea kwa nini hufanikiwi kufikia malengo yako ya kupata mimba.
Utajifunza njia mbalimbali za kimatibabu ambazo hutumika na madhara yake. Hivyo unaweza kuchukua maamuzi sahihi kwa kutumia njia sahihi na ukafikia malengo mapema
Utajifunza uko katika kundi gani la wanawake wanaotafuta mtoto ili ujue namna ya kujinasua na mtego wa kukosa maarifa
Mafunzo haya yanatolewa kwa njia ya mtandao kwa whatsapp na Telegram. Utakuwa unajisomea kwa muda wako wa ziada [Ambao hauna kazi].
Utaweza kujitibu tatizo hili la uzazi kwa kutenga muda hata wa nusu saa tu kila siku.
Kama unajiunga kuja kuangalia mafunzo na kuyaacha. Kama unalengo hilo tunza hiyo pesa nenda katoe sadaka kwa wahitaji. Usiendelee kutoa pesa usiyonufaika nayo.
Usiyependa kuyafuta uliyonayo ambayo hayajakupa matokeo.Kisha uweke maarifa mapya yatakayo kusaidia kwa safari ambayo unataka kuanzisha.
Kama hauko tayari elimu hii kuipokea,kuiamini na kuitekeleza kwa imani yote.
Mwanzo Mafunzo yetu ilikuwa 530,000
Sasa Lipia 30,000 Tsh tu. Leo Uanze mafunzo
Mafunzo ya awali kabla ya utekelezaji unatakiwa kujifunza siku 7 hadi 10. Baada ya kumaliza kujisomea majarida,video,audio na makala za mwongozo. Utaanza utekelezaji kwa vitendo. Sisi tumekuwekea malengo ndani ya miezi 4 hadi 6 wanafunzi wetu wengi huwa wameshafanikiwa kupata ujauzito. Lakini hautatolewa kwenye group letu.
This site is not a part of the Facebook website or Facebook Inc. Additionally, This site is NOT endorsed by Facebook in any way. FACEBOOK is a trademark of FACEBOOK, Inc.